Harmonize Aonyesha Mpenzi Wake Mpya wa Australia na Kuacha Kumfuata Kila Mtu Kwenye Instagram

Mwimbaji wa Tanzania Harmonize na mpenzi wake mpya kutoka Australia Briana; ndio wanandoa wa hivi punde mjini.Hivi karibuni Harmonize alimtambulisha Briana kwa mashabiki wake mtandaoni kwa kusambaza picha zake kadhaa kwenye akaunti yake ya Instagram, zikiwa zimeambatana na ujumbe mzito kwake.  

Katika ujumbe huo, Harmonize alisema alikuwa akisubiri kwa hamu kumuonyesha na kumjulisha jinsi alivyokuwa na maana kubwa kwake.

"Nimesubiri wakati huu kumwambia kila mtu unachomaanisha kwangu. Nataka tu kukupenda katika maisha haya na kuheshimu kila mwanamke. Ahadi kuwa huko kwa maisha yako yote. Karibu katika ulimwengu wangu malkia wangu” Harmonize aliandika. Harmonize pia ali-unfollow kila mtu kwenye Instagram yake isipokuwa Briana na kusema kuwa anataka tu kufuata mapenzi ya maisha yake. Aliongeza kuwa watu aliowa-unfollow wasiudhike kwani bado anawapenda na kuwaheshimu. "Ninapenda kila mtu huko nje lakini nataka tu kumfuata mwanamke wa maisha yangu. Kwa hivyo usijisikie kama sikupendi na kukuheshimu baada ya kutokufuata. You mean a lot to my life” aliandika Harmonize siku moja kabla ya ku-unfollow kila mtu.


Comments