Sosholaiti Vera Sidika Ajigamba Kwa Kuzuia Watu 2000 kutoka kwenye Instagram yake

Sosholaiti Vera Sidika hivi majuzi alifichua kuwa aliwafungia watu 2000 kwenye Instagram yake kwa siku moja.

Mrembo huyo alisema amechoshwa na watu wanaofuatilia ukurasa wake kumkosoa na kumsema vibaya.

Vera alisema kuwa anapendelea kuwa na wafuasi wachache kuliko kundi la watu wanaotarajia machapisho yake ili waweze kutaja ubaya. "Wafungwa 2000 waliingia kizuizini leo. Ikiwa huwezi kujali biashara yako nitakusaidia kuijali. Huwezi kumfuata mtu ili tu kuongea au kuchukia,” aliandika Vera.
Vera pia aliwaonya wale aliowazuia kuacha kumwomba mumewe amshawishi kuwafungulia.Alisema kuwa wengi wao wanadai kuwa hawana hatia.

Vera aliongeza kuwa wanaodai kuwa aliwafungia bila sababu hawana hatia kwa sababu alifanya hivyo baada ya kuona maoni waliyoandika sehemu nyingine.
"Ni afadhali kuwa na wafuasi 3 kuliko kundi la wafuatiliaji wanaosubiri kuona ninachochapisha ili wachukie. Acha kutuma DM kwa Brown ukimtaka anishawishi nikufungulie. Ati hukufanya kosa lolote,” aliongeza.


Comments