Sosholaiti Vera Sidika Aonyesha Uso wa Binti yake Mrembo kwa Mara ya Kwanza

Sosholaiti Mkenya Vera Sidika aliwashangaza mashabiki wake mchana wa leo baada ya kumuonyesha bintiye na Brown Mauzo Princess Asia Brown.

Vera alivunja mashaka kwa kushiriki picha nzuri ya Princess Asia Brown kupitia chapisho kwenye Instagram yake. Alisindikiza picha hiyo na maelezo ya utangulizi yenye kupendeza ambapo alimtaja binti yake kuwa zawadi kutoka kwa Mungu.
“Mungu ametupa kipande chake cha mbinguni. Kutana na Asia Brown” Alinukuu picha hiyo.
 

Ni mara ya kwanza kwa Vera kuwapa mashabiki picha ya binti yake mrembo tangu kuzaliwa. Vera na Mauzo Brown walitangaza kuzaliwa kwa binti yao mnamo Oktoba. Wanandoa hao hawakufichua uso wa mtoto wao licha ya kushiriki picha kadhaa za tarehe ya kujifungua.
Vera aliwashangaza mashabiki wake na ufichuzi huo kwa sababu chapisho lake linakuja wiki chache baada ya kuwaambia mashabiki wake kwamba angeanika uso wa binti yake mwaka ujao. Walakini, inaonekana kama alikuwa na mabadiliko ya moyo.

Comments