"Mimi sio mchawi" Zari Hassan Amlipua Mwimbaji wa Kenya Bamboo na Mkewe wa Uganda


Mwanasosholaiti wa Uganda, Zari Hassan, amemkashifu mwimbaji wa Kenya Timothy Kimani, anayejulikana kwa jina la Bamboo, na mkewe Erica Kimani kwa kusambaza uwongo kumhusu.

Katika mfululizo wa jumbe kwenye Snapchat yake, Zari alimkemea Erica na Bamboo na kuhoji kwa nini walikuwa wakisambaza uwongo kumhusu kwenye televisheni ya kitaifa. Hata hivyo, kile ambacho Zari hajui ni kwamba kipande cha video kinachosambaa mtandaoni kilitoka kwenye kituo cha YouTube cha Erica na Bamboo ambapo wanazungumzia mapambano yao na ibada ya shetani.

Kipande hiki cha video kilipakiwa tarehe 9 Juni 2023 kwenye kituo cha Erica na Bamboo. Katika video hiyo, Erica na Bamboo walimshutumu Zari kwa kuwa kala ya shetani kutoka ufalme wa baharini. Waliongeza kwa kudai jinsi alivyomuua mumewe na kuchukua mali yake. Erica pia alidai kuwa Zari bado anaajiri watu kwenye ufalme wa baharini. Inaonekana kama Zari amepata habari za tuhuma hizi, ndio maana amekasirika kwenye mitandao ya kijamii.

“Ekyenaku this is someone’s father, brother, husband on national TV selling lies. The disgrace nswala on your behalf. And someone’s mother, auntie, granny, sister to mention but a few. Muswaza plus the TV station that allows such nonsense, walahi your clowns. 2 grown ass adults. Please don’t bring me to your circus.” Zari aliandika kwenye Snapchat pamoja na picha ya video ya Bamboo na Erica inayosambaa.

Hadi sasa, hakuna Erica wala Bamboo aliyemjibu Zari. Na wakati watakapofanya hivyo, nitahakikisha nawajulisha.

Vinginevyo, niambie unafikiria nini kuhusu hali hii? Je, umewatch ushuhuda wa Bamboo na Erica? Ikiwa umefanya hivyo tafadhali shiriki mawazo yako kwenye sehemu ya maoni.

Comments