"Akaniambia nipige picha za uchi" Shorn Arwa Afunguka kuhusu kukutana kwake na mwanamume maarufu

MwanaYouTube wa Kenya, Sharon Arwa, almaarufu Shorn Arwa, amefunguka kuhusu kukutana na mtumbuizaji maarufu wa Kenya katika siku zake za awali katika tasnia ya burudani.

Huku akieleza kwanini hafanyi kazi na baadhi ya mapromota na wasanii katika tasnia hiyo, Shorn Arwa aliwaambia mashabiki wake kwamba aliwahi kuwa na uzoefu wa kutisha na mtu mashuhuri wa kiume katika uwanja huo.

Mtayarishaji wa maudhui alifichua kwamba aliwasiliana na Mtu Mashuhuri wa kiume na akaomba ushirikiano wa kazi ili kusukuma kazi yake. Hata hivyo, chaguo alilompa lilimshtua sana.

Shorn Arwa alifichua kuwa Mtu Mashuhuri alipendekeza wampige picha za uchi na kuzivujisha ili kupata wafuasi wengi.

“Kuna mtu aliniuliza kwa nini sifanyi vitu na baadhi ya mapromota na wasanii kwenye tasnia. Wakati huo, kulikuwa na mtu huyu, uso wa burudani zaidi na yote kati ya wavulana ambao wanasimamia. Nilikuwa kama yo, niunganishe tufanye kitu. Tufanye kazi pamoja”  

“Huyu jamaa alifungua tu mdomo wake na kusema kwamba ni kwa sababu ninajifanya niko mkali lakini katika maisha halisi mimi si mkali na siku willing kutake risks. So nikamwambia mimi natake risks. Ikiwa inahusika na pesa tuchukue hatari pamoja" “Imagine huyu mkebe anafungua tu mdomo na kuniambia kwa mfano wewe sasa leo tukitaka uchukue picha za uchi halafu tufanye kiki utakubali. Nilikuwa kama nini? Saa hizi tunaweza tu kupiga picha nzuri na kisha tunajifanya na kuzivujisha, halafu upate trafiki,” alieleza Shorn Arwa kwenye video iliyopakiwa mtandaoni. Licha ya kufunguka kuhusu tukio hili, Shorn Arwa hakufichua utambulisho wa mtu mashuhuri.

Comments